Umma wa Wapanda Baisikeli Dar es Salaam
(UWABA)

Katiba

    Jina

  1. Jina la Umma ni Umma wa Wapanda Baiskili Dar es Salaam (UWABA)

    Kwa mawasiliano

  2. Umma utafungua sanduka la posta kwa ajili ya mawasiliano na katibu atakuwa na ufunguo. Aidha, simu ya katibu wa kamati itatumika kama simu ya Umma.

    Ufafanuzi

  3. Baisikeli ina maana ni mashini ya usafiri ambao hautumii injini, na unatumia tairi (wheels), pedali na mnyororo.
  4. Umma ina maana Umma wa Wapanda Baiskili Dar es Salaam

    Malengo

  5. Malengo ya Umma ni kama yafuatavyo:
    1. Kuhamasisha watu wa Dar es Salaam kutumia baisikeli
    2. Kuhamasisha wanawake kupanda baisikeli
    3. Kufanya utafiti kupata taarifa kuhusu wapanda baisikeli na maoni yao
    4. Kushirikiana na serikali na kuhamasisha na kuwashauri kuweka huduma kwa wapanda baisikeli na kuweka mazingira mazuri na salama kwa wapanda baiskeli (mfano sehemu maalumu ya barabara hasa kwa baisikeli, sehemu za kupaki baisikeli, sehemu za kuoga baada ya kupanda baisikeli)
    5. Kuhamasisha na kuwashauri serekali kuweka mazingira mazuri na salama kwa usafirishaji wa mizigo kwa baisikeli
    6. Kushirikiana na mashirika mengine ambayo yana malengo kama haya
    7. Kuhamasisha waendesha magari kuheshimu na kuwapa nafasi wapanda baisikeli na kuwapa haki zao barabarari
    8. Kuhamasisha wapanda baisikeli kuendesha salama, mfano kutumia taa usiku, kutumia kofia ngumu (helmet) na kujua sheria za barabarani
    9. Kuwasaidia watu ambao wameumizwa na waendesha magari wakati wa kupanda baisikeli ili kupata fidia zao.

    Kujiunga

  6. Wanachama wawe kama ifuatavyo:
    1. Watu ambao wanapanda baisikeli kawaida mjini au wazazi wa watoto ambao wanapanda baisikeli kuenda shuleni
    2. Wanaokaa Dar es Salaam au karibu na Dar es Salaam
    3. Watu ambao wana malengo kama ilivyoandikwa hapo juu
  7. Hakuna ada ya kujiunga wala ada ya kila mwaka. Michango itakuwa siyo lazima na kwa ajili ya malengo maalumu
  8. Mtu atalazimika kuacha kuwa mwanachama kama:
    1. mkutano wa Umma utamuona hana malengo kama yalivyoandikwa hapo juu; au
    2. ataiba pesa ya Umma au atatumia vibaya pesa za Umma; au
    3. ana kesi ya jinai ya muhimu

    Kamati

  9. Kamati ya Umma itakuwa ina watu watano ambao ni wanachama.
  10. Mmoja atakuwa Mwenyekiti, mmoja Katibu, mmoja Mweka Hazina na wawili wa kawaida.
  11. Mwenyekiti atakuwa na uwezo wa kuita mikutano ya Umma na atakuwa mwenyekiti wa mkutano.
  12. Mweka Hazina atakuwa na wajibu wa kuhesabu pesa zote za Umma na kuandika pesa inayoingia na matumizi yake yote. Wanachama watakuwa na haki ya kuangalia taarifa hii.
  13. Katibu atafanya mawasiliano na wanachama na watu wengine. Aidha, atanadika maamuzi ya mikutano, atafanya kazi ya utawala, na atachukua nafasi ya mwenekiti kama hayupo.

    Mikutano ya Umma

  14. Mkutano wa Umma unaweza kuitwa na Mwenyekiti, au kuitwa na zaidi ya wanachama kumi ambao wamewaambia kamati wanataka mkutano
  15. Katibu atawasiliana na wanachama wote ambao wana sanduka la posta au simu kuhusu mkutano zaidi ya siku mbili kabla ya mkutano, na ataweka matangazo kuhusu mkutano
  16. Mkutano unaweza kuondoa kamati kama zaidi ya nusu wanakubali.
  17. Mkutano unaweza kupiga kura kuchagua kamati mpya kama kamati ya zamani imeondolewa au wanaweza kuchaguo mtu mpya kwa nafasi ya kamati kama mwenye nafasi hii ameiacha
  18. Mkutano unaweza kufanya maamuzi na maoni mbalimbali kama zaidi ya nusu ya mkutano wanakubali.
  19. Mkutano unaweza kuunda kamati ndogo ndogo kushugulikia mambo Fulani, mfano kamati ndogo ya utendaji.

    Mikutano ya kamati

  20. Kamati watakutana mara kwa mara kwa ajili ya kufanya kazi ya kawaida ya Umma
  21. Kama kamati hawakubaliani kuhusu mambo muhimu, mwenyekiti ataita mkutano wa Umma kufanya uamuzi.

    Mambo ya pesa

  22. Pesa itatoka michango ya wanachama, ya watu wengine, ya vyama vingine na ya mashirika mengine ambao wana malengo kama yalivyoandikwa hapo juu

    Kubadilisha katiba

  23. Katiba inaweza kubadilishwa kama zaidi ya 75% ya wanachama wanakubali kubadilisha katiba ndani ya mkutano au kwa kuandika barua

    Kuvunja UWABA

  24. UWABA inaweza kuvunjwa kama zaidi ya 75% ya wanachama wanakubali
  25. Kama UWABA itavunjwa, mali na pesa za UWABA zitahamishiwa kwenye shirika lingine ambalo lina malengo yanayofanana na malengo ya UWABA

    Rudi nyuma