Raphaeli - New
famous Chagga rap!
Ni namna gani ah, ni jinsi gani tutawini maishani
mpaka siku tunasema buriani, ah x3
Ilikuwa Jumapili nkamuona Raphaeli, amekaa juu ya
nini, ni juu ya baiskeli,
namuuliza anaenda wapi kaniambia anaenda feri,
Huko feri ni kwa
nani, kwa lile jitu tapeli,
sasa utamuona wapi, atakuwa kwenye meli,
kwenye meli ndo
wapi, ndo huko huko feli
Baadaye namuona huyo huyo Raphaeli
anacheza na nani,na yule dada Mary,
namuuliza Raphaeli hapa ndiyo feri,
anasema siyo
hivyo,mwenziyo unajua nimeharibikiwa na ile baiskeli, nategemea kwenda
kule Oysterbay,
nako huko
ntamkuta brother Mtei,
yeye ndiyo atakayenipunguzia bei ya spea za baiskeli
Ah, Ni namna gani ah, ni jinsi gani tutawini maishani
mpaka siku tunasema buriani, ah x3
Kesho yake nikatoka moja kwa moja kwa Raphaeli,
nikamkuta nyumbani anasikiliza CD ya R. Kelly,
nkamuuliza Raphaeli unayo CD ya Makafeli,
akaniambia na Makafeli, R. Kelly na Mariah Carey
Sisi hatukukaa,
Tukatoka moja
kwa moja haooo, mpaka kwenye baa
unaambiwa watu walikuwa wamejaa,
Kengeleki
zimeshikamanan,baiskeli na motocar,
Basi tukaagiza masanga pale na kiti moto tukaanza
kupata moja baridi moja moto
wakati tunaendelea eeeh,
kidogo tu huyooo
katokea mzee Urassa
na ile
Land Cruiser yake new model ya kisasa power engine 2.4,
filling system ya kisasa,
unaambiwa ni automatic kuanzia viti hadi vitasa
Basi alikuwa na laki tatu mfukoni, akajishika kiunoni
akatuangalia usoni,
akatudharau akaingiza mkono mfukoni
akatoa pesa
akaweka pale mezani kisha akaenda chooni
Sisi basi tukaanza kulewa, tukalewa tukalewa, yesu
wangu,
tulilewa tulilewa tulilewa tulilewa, wakaongezeka ndugu zetu kutoka
sehemu mbalimbali za kilimanjare, Marangu, Machame, Uru, Kishmoto,
Kibosho,Mwika, Mbunju mpaka Kiborloni,
unaambiwa
Tarakea mpaka huku sehemu za Rombo,
wote pale wakawa wamemiminika,
Masawe alikuwepo, Mariale alikuwepo,Shirima
alikuwepo, Mangi
alikuwepo, Mrema alikuwepo, Ndosi alikuwepo, Mlei alikuwepo, Asei
alikuwepo,mama Prisca alikuwepo, mama Manka alikuwepo, Minja
alikuwepo, Kiluwa alikuwepo, na huyo mtoto anakaa mtaa wa pili nani?
Chuwa,eti Chuwa naye alikuwepo
Ni namna gani ah, ni jinsi gani tutawini maishani
mpaka
siku tunasema
buriani, ah x3
Wakati tunaendelea kupata pale masanga na kiti moto,
Raphaeli na Masawe haooo, wakatoka
sikujua kinachoendelea, nikajua wanaenda kuruka majoka
kwa sababu kulikuwa na mziki wa Reggae, charanga na ule mziki wa
kufokafoka.
Akilini mwangu
nilikuwa nafikiri kwamba mambo yataenda yakifanya
nini,yakienda yakinyooka.
Kumbe huko walikokwenda
walienda kuwachokoza wake za watu wakawa wameketi,
wakaanza
kuwashikashika mabegani mpaka zile sehemu zao nyeti.
Basi waumbe zao
nikawaona wamechukia
maneno machafu
wakaanza kuwatupia,
Kinabo wewe,wacha mke wangu kima wewe
unamshikia nini huko, mara
huyu kamtukana mwezake
sijui kamwambia fala wewe, huyu kamrudishia maneno yale na lile,
basi tu
ikawa vurugu mechi.
Basi wale wanaume nikawaona wamebeba mawe
wakataka
wamponde nayo Masawe.
Basi Raphaeli akamrukia teke mmoja wao akamuangusha palepale.
Akataka akimbie
hajafika mbali akakamatawa na nani, na yule
afande Charle,
Asa mie
nikamuambia afande Charle, naomba basi umruhusu huyu
Raphaeli nyumbani akalale.
Akaniambia ni
lazima kituoni huyu Raphaeli leo akalale,
Sasa nikaona
sina tena la kufanya,
Raphaeli ndo
huyo tena amesha ulowanya.
Kwanza mimi kichwani lager zishanchanganya ikabidi tungoje
kesho tu tujue ni kitu gani tutafanya.
Basi kama
Raphaeli ndo kama ameua,
basi pesa zangu zote polisi watakuwa wamechukua,
yesu wangu,
yelleeuwiii
Pesa ni maua maana maua hunyauka, vile vile huchanua
Ah, Ni namna gani ah, ni jinsi gani tutawini maishani
mpaka siku tunasema
buriani, ah x3